RAIS RUTO AFANYA MABADILIKO MAKUBWA KATIKA UONGOZI WA KDF, ATEUA VIONGOZI WAPYA NA KUPANDISHA VYEO MAAFISA.
By Dayo Radio
Published on 05/06/2026 15:17
News

Rais William Ruto amefanya mabadiliko makubwa ndani ya uongozi wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), yakihusisha uteuzi wa maafisa wapya, upandishaji vyeo na kuongezewa muda wa utumishi kwa baadhi ya viongozi wa jeshi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka wizara ya linzi, mabadiliko hayo yamefanyika kufuatia mapendekezo ya Baraza la ulinzi na yanalenga kuimarisha ufanisi wa uongozi na utendaji kazi ndani ya jeshi.

Katika uteuzi huo, Meja Jenerali John Maiso Nkoimo ameteuliwa kuwa Naibu Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu (Kenya Army), akichukua nafasi ya Meja Jenerali Mohamed Nur Hassan ambaye amestaafu.

Aidha, Brigedia Mohamud Salah Farah ameteuliwa kuwa Naibu Kamanda wa Jeshi la Wanahewa (Kenya Air Force), huku maafisa wengine kadhaa wakipandishwa vyeo na kupewa majukumu mapya katika vitengo mbalimbali vya jeshi.

Rais Ruto pia ameongeza muda wa utumishi wa Kamanda wa Jeshi la Majini, Meja Jenerali Paul Owuor Otieno, kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kuendelea kuimarisha uongozi na utekelezaji wa majukumu katika kikosi hicho.

Wizara ya Ulinzi imesema kuwa mabadiliko hayo ni sehemu ya juhudi za serikali za kuimarisha uwezo wa KDF katika kutekeleza majukumu yake ya kulinda usalama wa taifa na maslahi ya wananchi.

 

NA HARRISON KAZUNGU.

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online