NCIC YATOA ONYO KALI KWA WANAOTOA MATAMSHI YA CHUKI NA UKABILA.
By Dayo Radio
Published on 26/05/2026 13:32
News

Tume ya uwiano na utangamano wa Kitaifa, NCIC, imetoa onyo kali kwa wanasiasa wanaotoa matamshi ya chuki na ukabila kufuatia matamshi ya hivi majuzi ya Katibu Mkuu wa chama cha UDA. Akizungumza na wanahabari, Mwenyekiti wa tume hiyo Dkt. Keffa Omaye amesema kumekuwa na ongezeko la matamshi ya kuwagawanya Wakenya kwa misingi ya kikabila na kisiasa, hali ambayo inaweza kuhatarisha amani, mshikamano na utulivu wa taifa.

Omaye amesema viongozi wana wajibu wa kutumia majukwaa yao kuhubiri umoja wa kitaifa, mshikamano na kuendeleza amani badala ya kutoa kauli za uchochezi zinazoweza kuleta migawanyiko miongoni mwa wananchi.

Aidha, ameonya kuwa tume hiyo haitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya yeyote atakayepatikana akikiuka sheria za uwiano na utangamano nchini bila kujali nafasi yake katika jamii au mrengo wake wa kisiasa.

Wakati huo huo, NCIC imewataka wananchi kushirikiana na mamlaka husika kwa kuripoti matamshi ya chuki na uchochezi ili kusaidia kudumisha amani na utangamano nchini hasa wakati huu wa joto la kisiasa.

Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa, NCIC, imetoa onyo kali kwa wanasiasa wanaotoa matamshi ya chuki na ukabila kufuatia matamshi ya hivi majuzi ya Katibu Mkuu wa chama cha UDA.

Akizungumza na wanahabari, Mwenyekiti wa tume hiyo Dkt. Keffa Omaye amesema kumekuwa na ongezeko la matamshi ya kuwagawanya Wakenya kwa misingi ya kikabila na kisiasa, hali ambayo inaweza kuhatarisha amani, mshikamano na utulivu wa taifa.

“Viongozi wana wajibu wa kutumia majukwaa yao kuhubiri umoja wa kitaifa na kudumisha mshikamano wa wananchi badala ya kutoa matamshi ya uchochezi yanayoweza kugawa taifa,” amesema Omaye.

Aidha, ameonya kuwa tume hiyo haitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya yeyote atakayepatikana akikiuka sheria za uwiano na utangamano nchini bila kujali hadhi yake kisiasa au kijamii.

“NCIC haitamuonea haya yeyote atakayepatikana akieneza matamshi ya chuki. Sheria itachukua mkondo wake bila upendeleo,” ameongeza.

Wakati huo huo, tume hiyo imewataka wananchi kushirikiana na mamlaka husika kwa kuripoti matamshi ya chuki na uchochezi ili kusaidia kudumisha amani na utangamano nchini hasa kipindi hiki cha joto la kisiasa.

NA HARRISON KAZUNGU.

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online