FURAHA KWA ARSENAL
By Dayo Radio
Published on 20/05/2026 10:10
News

Baada ya kusubiri kwa muda wa miaka 22, hatimaye Arsenal wametwaa rasmi ubingwa wa Premier League msimu wa 2025/26, hatua inayowarejesha kileleni mwa soka la England kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004.

 

Ubingwa huo umethibitishwa rasmi usiku wa kuamkia leo baada ya Manchester City kulazimishwa sare ya mabao 1-1 dhidi ya Arsenal, matokeo yaliyoifanya City kubaki na pointi 78 na kushindwa kuifikia Arsenal ambao wanaongoza msimamo kwa alama 82.

 

Mafanikio hayo yanaashiria mwisho wa kipindi kigumu kwa Arsenal, ambao kwa misimu mitatu mfululizo walimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Manchester City. Chini ya uongozi wa kocha Mikel Arteta, klabu hiyo imeonyesha mabadiliko makubwa kupitia nidhamu, soka la kuvutia na kujenga kikosi imara kilichoweza kushindana kwa kiwango cha juu hadi kutwaa taji hilo muhimu.

 

Ubingwa huu pia unaweka historia mpya kwa Arsenal, ambao sasa wanatajwa tena miongoni mwa vilabu vinavyotawala soka la England baada ya miaka mingi ya kusubiri na kukosa mafanikio ya ligi kuu.

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online