GHASIA ZASABABISHA USAFIRI KUSITISHWA KATIKA DARAJA LA NYALI
By Dayo Radio
Published on 18/05/2026 13:32
News

Msongamano mkubwa wa magari umeshuhudiwa katika Daraja la Nyali baada ya magari kadhaa kulazimika kurejea mjini kutokana na hali ya sintofahamu iliyotokea eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mashuhuda, baadhi ya matatu na tuktuk zimeripotiwa kupigwa mawe na watu wasiojulikana, hali iliyozua hofu miongoni mwa wasafiri na madereva.

Maafisa wa usalama wameelekezwa eneo hilo huku juhudi za kurejesha utulivu na kuhakikisha usalama wa watumiaji wa barabara zikiendelea.

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online