Mwimbaji wa nyimbo za injili Rachel Wandeto ambaye alipata umaarufu baada ya kujichora picha ya Rais William Ruto ameaga dunia.
By Dayo Radio
Published on 18/05/2026 12:46
News

Mwimbaji wa nyimbo za injili Rachel Wandeto ambaye alipata umaarufu baada ya kujichora picha ya Rais William Ruto ameaga dunia.

 

Rachel alikuwa amelazwa katika hospitali kuu ya Kenyatta akipokea matibabu ya majeraha makubwa ya moto baada ya kudaiwa kumwagiwa petroli na kuchomwa moto na watu wasiojulikana katika eneo la Mwiki.

 

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, Rachel alivamiwa na wanaume watatu waliokuwa wameficha nyuso zao waliomtuhumu kupokea fedha kutokana na kumuunga mkono Rais Ruto. Inadaiwa wanaume hao walitaka pesa, na baada ya kusema hana, walimwagia petroli na kisha kumchoma moto kabla ya kutoroka. 

 

Tukio hilo limezua huzuni na hasira miongoni mwa Wakenya huku viongozi na wanamuziki wakilaani shambulizi hilo. 

 

Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen alitembelea hospitalini na kuahidi uchunguzi wa kina ili waliohusika wakamatwe.

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online