Serikali ya Kaunti ya Mombasa imezindua rasmi ujenzi wa Hospitali ya Kongwea Level 4 , eneo Bunge la Nyali.
By Dayo Radio
Published on 27/04/2026 17:41
News

Akizungumza Katika hafla hiyo Gavana wa Kaunti ya Mombasa Abdulswamad Sharrif Nassir amesema Hospitali hiyo ambayo imepewa jina la 'Raila Odinga Level 4 Hospital' itasaidia pakubwa Katika kurahisisha utoaji na upatikanaji wa huduma za Afya Kwa wakaazi wa eneo Bunge la Nyali na viunga vyake.

Gavana Nassir amesema ujenzi wa Hospitali hiyo utagharimu Milioni 250 na sasa serikali ya Kaunti hiyo inalenga Kujenga hospitali nyingine 3 sawia na hiyo sehemu tofauti Kaunti ya Mombasa.

Gavana wa Kaunti ya Homa Bay Gladys Nyasuna Wanga aliyeandamana na gavana Nassir amesifia Mradi huo akisema viongozi wa ngazi zote wana jukumu la Kutoa huduma Bora Kwa watu na kuangazia Kwa kina Maendeleo Kwa faida ya watu wanaowawakilisha .

Mwenyekiti huyo wa Chama Cha Chungwa amepuzilia mbali Kauli za baadhi ya viongozi wa Kundi la LindaMwananchi wanaojitwika nyadhifa za uongozi wa chama Cha ODM pasi kufuata taratibu zilizopo na sheria za chama hicho.

Wanga amesisitiza ndoa ya ODM na UDA Bado haijangia doa na hivi karibuni vyama hivyo viwili vitaaanza mazungumzo rasmi ya namna viunda muungano wa Kisiasa kabla ya uchaguzi Mkuu wa 2027.

Kauli ya viongozi hao inajiri huku mgogoro wa uongozi ukizidi Kutokota ndani chama Cha Chungwa; huku Makundi ya Linda Mwananchi na Linda Ground yakitofautiana na kuleta migawanyiko zaidi chamani.

Comments
Comment sent successfully!