Nassir Aweka Jiwe la Msingi wa Hospitali ya Kongowea Level 4 Mombasa
By Dayo Radio
Published on 27/04/2026 16:07 • Updated 27/04/2026 17:33
News

Nassir Aweka Jiwe la Msingi wa Hospitali ya Kongowea Level 4 Mombasa

 

 

Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir mapema leo ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Kongowea Level 4, mradi unaotarajiwa kugharimu takriban shilingi milioni 250. Hatua hiyo inalenga kuboresha huduma za afya kwa wakazi wa Kongowea na maeneo ya karibu.

 

Akizungumza katika hafla hiyo akiwa ameandamana na baadhi ya viongozi wa kaunti, Nassir amesema hospitali hiyo itaitwa Raila Odinga Kongowea Hospital. Ameeleza kuwa kituo hicho kitakuwa miongoni mwa hospitali kuu katika ukanda wa pwani, na kuongeza kuwa kuna hospitali nyingine zinazoendelea kujengwa ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa haraka na kwa ufanisi.

 

“Lengo letu ni kuhakikisha wananchi wa Mombasa wanapata huduma bora za afya bila kuchelewa. Hospitali hii ya Kongowea itakuwa miongoni mwa vituo vikuu vya afya katika ukanda wa pwani, na tunaendelea pia na miradi mingine ya hospitali ili kuboresha huduma hizi".

 

Wakati uo huo Mwenyekiti wa chama cha ODM ambaye pia ni Gavana wa Homa Bay, Gladys Wanga, amewakosoa vikali viongozi wa upinzani akiwataka kuzingatia kuleta maendeleo kwa wananchi badala ya kuendeleza siasa za ukabila. 

 

“Viongozi wanapaswa kuacha siasa za mgawanyiko na badala yake kuzingatia maendeleo ya wananchi. Wakenya wanahitaji huduma na maendeleo si siasa za ukabila.

 

Kauli ya Mwenyekiti huyo inajiri siku siku chache baada ya ziara ya viongozi wa upinzani Ukanda wa Pwani ambapo walikashifu viongozi wa serikali Kuu Kwa kukosa kutekeleza ahadi zao Kwa Wakenya huku wakimsuta Gavana Nassir Kwa Kutelekeza Hospitali ya Makandara wakisema uongozi wake umekosa dira.

Comments
Comment sent successfully!