Kampuni kubwa zaidi duniani ya kutengeneza mipira ya kondomu imeonya kuhusu kuongezeka Kwa bei za bidhaa hizo kufuatia athari za vita vinavyoendelea kati ya Iran na mataifa ya Magharibi.
Kwa mujibu wa taarifa , ongezeko hilo la bei linatokana na changamoto za usambazaji wa bidhaa, hasa njia kuu za usafirishaji wa kimataifa zinazopita katika maeneo yaliyoathirika na mzozo huo.
Aidha, kupanda kwa bei ya mafuta kumesababisha kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wa malighafi zinazotumika kutengeneza kondomu, hali inayowalazimu wazalishaji kupandisha bei ili kuendana na hali ya soko.
Wataalamu wa sekta ya afya ya uzazi wanasema huenda ongezeko hilo likaleta changamoto kwa upatikanaji wa kondomu, hasa katika nchi zinazoendelea kutegemea misaada na bei nafuu.
Hata hivyo, kampuni hiyo imesema inaendelea kufuatilia hali ya soko na kutafuta njia za kupunguza athari kwa watumiaji.