Mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika Kaunti ya Mombasa imesababisha mafuriko makubwa katika eneo la Bamburi hali iliyosababisha athari kwa biashara nyingi pamoja na miundombinu ya kijamii.
mzee wa mtaa wa kadzandani John Simba Mwaigho ametoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kudhibiti hali hiyo kabla haijazidi kuwa mbaya na kusababisha maafa zaidi.
Aidha baadhi ya wakaazi wa eneo hilo wameitaka serikali ya kaunti kuingilia kati kwa dharura wakisisitiza umuhimu wa kuwekwa kwa mifumo bora ya maji taka na mifereji ya kupitisha maji ili kupunguza hatari ya mafuriko siku zijazo.
Wakaazi hao wameeleza wasiwasi wao kuhusu usalama na afya wakihofia kuenea kwa magonjwa endapo hatua stahiki hazitachukuliwa kwa wakati.