Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewataka maafisa wa serikali na viongozi katika msafara wake kutumia basi moja kutokana na uhaba wa mafuta unaolikumba taifa hilo.
Akizungumza na wanahabari, rais Suluhu amesema kuwa hatua hiyo inalenga kuhakikisha nchi inaokoa akiba ya mafuta ambayo imeathiriwa na vita vinavyoendelea katika eneo la Mashariki ya kati.
Hata hivyo Amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila kiongozi serikalini kuonyesha mfano kwa wananchi katika matumizi bora ya rasilimali, hasa wakati wa changamoto za kiuchumi.