IDARA YA USALAMA ILIVURUGA MKUTANO WETU" VIONGOZI WA MRENGO WA LINDA MWANANCHI.
By Dayo Radio
Published on 30/03/2026 06:42
News

Viongozi wa mrengo wa Linda Mwananchi ndani ya chama cha ODM, pamoja na wafuasi wao, wamekosoa vikali idara ya usalama kwa kuvuruga mkutano wao wa kitaifa uliofanyika katika ukumbi wa Ufungamano House jijini Nairobi.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, naibu kiongozi wa ODM Godfrey Osotsi, Gavana wa Siaya James Orengo, na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino.

“Polisi wamevuruga mkutano wetu na kutibua amani, jambo ambalo halikubaliki kwa chama kinachodai kuenzi demokrasia,” amesema Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna.

Hali hii inatokea huku kuna mgawanyiko ndani ya chama cha ODM, ambapo mrengo wa Linda Mwananchi umeandaa mkutano mwingine katika viwanja vya Jamhuri. Viongozi hao wamesisitiza

 “Tunataka maoni yetu ya kisiasa yaamuliwe kwa heshima, na mikutano yetu ifanyike kwa amani bila vurugu za aina yoyote.”

Wafuasi wa mrengo huo wamesema kuwa hatua ya polisi ilikuwa ni “kukatisha tamaa na kuingilia uhuru wa kisiasa wa chama,” huku wakitoa wito kwa vyombo vya usalama kuhakikisha heshima na utulivu unadumishwa katika mikutano yote ya kisiasa.

 

NA HARRISON KAZUNGU.

Comments
Comment sent successfully!