UTABIRI WA HALI YA HEWA MOMBASA
By Dayo Radio
Published on 03/02/2026 17:03
News

Na Elijah Muthini 

Hali ya ukame inatarajiwa kutawala katika kipindi chote cha wiki hii (3-9 Februari) ingawa baadhi ya maeneo yanaweza kushuhudia mvua nyepesi asubuhi katika siku chache. Kwa ujumla, hali ya hewa itaendelea kuwa tulivu na yenye joto la wastani.

Joto la juu wakati wa mchana linatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 31-33°C, huku joto la chini likitarajiwa kufikia nyuzi joto 25°C hali itakayochangia kuwepo kwa hali ya hewa tulivu na ya kawaida. Upepo wa wastani unatarajiwa kuvuma kwa wiki nzima kwa kasi ya mita 7 hadi 8 kwa sekunde.

Hali ya bahari inatarajiwa kuwa ya wastani huku mawimbi yakifikia kati ya mita 1.0 hadi 1.5. Hali hii inahitaji umakini zaidi hasa kwa shughuli za uvuvi na safari za majini.

Wananchi wanahimizwa kuchukua tahadhari zinazofaa, hususan wanapojihusisha na shughuli za nje au baharini. Inashauriwa kunywa maji ya kutosha, kufuatilia taarifa za hali ya hewa mara kwa mara, na kuwa waangalifu wanapokuwa baharini.

Comments
Comment sent successfully!