Mashindano ya Qurani Nyali Kuanza Februari 7, 2026
By Dayo Radio
Published on 31/01/2026 17:10
News

Vijana wa eneo bunge la Nyali kaunti ya  Mombasa wamehimizwa kujitosa katika mashindano ya Quran yanayo tarajiwa kuanza tarehe 7 mwezi wa feb 2026 hatua inayolenga kukuza maadili mema na kupambana na uhalifu katika jamii.

Akizungumza katika kongamano hilo Sheikh Ali Mohammed, mkuu wa majaji wa mashindano hayo, amewahakikishia walimu na wanafunzi kuwa majaji watafanya uamuzi wa haki na waadilifu vile vile amesema kuwa wote watakaofuzu vizuri watatunzwa.

" Wanafunzi ambao watakaoshiriki na walimu wao nawaambia kuwa tutajitahidi kadri tofiki ya Allah  tufanye uadilifu katika ujaji wa musabaq huu kwa hivyo maustathi na wanafunzi wasiwe na wasiwasi. Watakavyokuwa wamestathi ndivyo watakavyowahukumu katika musabaq huu bila kuzingatia hawa watoka waeneo ama madrassa gani kwa sababu hatuangalii hayo katika madrassa hii.

Tutakachoangalia katika kuhukumu Musabaq huu ni usomaji wa Quran na watakaosoma kama inavyostahili pasi kuzingatia sauti zao watatunzwa."

Kwa upande wake Mgombea ubunge wa Nyali Elkana Jacob  ametoa wito kwa majaji na viongozi wa kidini kutilia maanani mafundisho ya dini ili kusaidia jamii kukabiliana na visa vya uhalifu vinavyoshuhudiwa mara kwa mara katika eneo hilo.

" Ninawaomba tafadhali majaji kupitia kwa kiongozi wao,Maimamu na Maustadhi tulichukulie hili jambo kwa nidhamu na kwa sababi ya kizazi chetu kijacho kwani watoto hawa tusipowalea vizuri wanapotoka kimaadili na kujishirikisha na mambo mabaya hivyo kuongezeka visa vya uhalifu. "

Comments
Comment sent successfully!