Vijana pamoja na wadau wa mazingira leo wameungana katika zoezi la kusafisha eneo la likon ferry kaunti ya mombasa wakitoa wito wa mshikamano katika kulinda mazingira na kupunguza uchafuzi katika njia hiyo muhimu ya usafiri.
Mkurugenzi wa shirika la Mombasa youth cousel Antigoals Ray, amesema lengo kuu la zoezi hilo ni kusafisha eneo ambalo limekuwa likitumika kama sehemu ya kutupa taka kinyume cha sheria huku akitoa wito kwa serikali na vijana kushirikiana ili kuhakikisha mazingira ya Likoni Ferry yanabaki safi na salama.

"We are passing this information to the county government and national government that's there is an illegal dumpsite here at likon and we want to clean it but through their support will make it easy for us to clean so that we can have a very productive tourism centre since this is the channe"
Kwa upande wake Katibu wa Mazingira na Uchumi samawati katika shirika hilo Magrete Mutuku amesema Likoni Ferry ni njia muhimu inayotumiwa na watoto wanaoenda shule pamoja na wafanyibiashara wadogo, akisisitiza kuwa mazingira safi ni muhimu kwa afya, usalama na maendeleo ya kiuchumi.
“Ningependa kuiomba serikali pamoja na mashirika ya kijamii kushirikiana nasi kusafisha Likoni Ferry kwa sababu hii ni channel muhimu sana kwa uchumi na maisha ya kila siku ya watu wetu.”

Hata hivyo mwenyekiti wa Likoni Waste Recycle Eid Mohammed, ameitaka serikali na wadau mbalimbali kushirikiana katika kutoa hamasisho la umuhimu wa mazingira safi hasa kwa wafanyibiashara wa eneo hilo ambao amesema wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kupunguza utupaji holela wa taka
“Tunaiomba serikali na washikadau mbalimbali kushirikiana nasi kutoawz hamasisho juu ya umuhimu wa mazingira safi, hasa kwa wafanyibiashara wa eneo hili kwa sababu wao ndio wahusika wakuu wa uchafuzi wa sehemu hii.”