UKOSEFU WA MBINU DHABITI WATAJWA KUWA KERO KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM.
By Dayo Radio
Published on 15/01/2026 08:48
News

Mwenyekiti wa Chama cha Kitaifa cha Wazazi (National Parents Association) Kaunti ya Mombasa Mikidadi Ahmed Abdallah ametoa wito kwa mashirika ya kijamii wadau wa elimu na wafadhili kujitokeza kusaidia wanafunzi walemavu wanaosoma katika shule za kuwaida.

Akizungumza na idhaa hii Ameeleza kuwa baadhi ya shule hazina miundombinu dhabiti za kuwasaidia wanafunzi walemavu akitaja uhaba wa vyoo maalum na njia za kupandia (ramps) ambazo ni muhimu huku akisema baadhi ya wanafunzi hao wanakabiliwa na changamoto za kifedha hali inayowafanya washindwe kumudu karo na mahitaji mengine ya shule.

"Zile facilities za infrastructure ambazo zinaeza kuwasuport examplaes the washroom ama stairs ambako some hawa ramps inakua changamoto kwao so am just appealing for members non Organization wajitolee wafike katika shule hizo wawasadie kujenga miuondo mbinu inayohitajika"

Aidha amewataka wadau mbalimbali kujitokeza na kusaidia shule kupata angalau baadhi ya walimu watakaopatiwa mafunzo maalum ya kushuhulikia wanafunzi wenye mahitaji maalum, ili waweze kuwasaidia endapo kuna changamoto itatokea shuleni

"Waende shule watrain iwe kukutokea emergency shuleni wanaweza kupeana huduma ya kwanza kabla kuenda hospital lakini kwa sasa ni changamoto maana hata walimu hawajui jinsi ya kuwasaidia kunapotekea changamoto wanapokua shuleni."

Comments
Comment sent successfully!