Na Elijah Muthini
Tunapoingia wiki ya kwanza mwezi wa Januari (tarehe 5–12 Januari 2026), kunatarajiwa kuwa na joto jingi yenye utulivu katika baadhi ya maeneo ya Mombasa, Kenya. Ukavu huu unatarajiwa kutawala kwa wiki nzima, hali itakayosaidia kwa shughuli za nje, matembezi pamoja na shughuli za kila siku. Hata hivyo, maeneo machache yanaweza kushuhudia mvua nyepesi za asubuhi, hasa katika mwendo wa alfajiri. Mvua hizi zinatarajiwa kuwa za muda mfupi na kuisha haraka kadri siku inavyoendelea.
️ Joto la mchana litaendelea kuwa juu, likiwa kati ya nyuzi joto 31–33°C, hali itakayofanya joto kuwa kali zaidi hasa wakati wa alasiri. Wakaazi wanashauriwa kunywa maji ya kutosha, kuvaa mavazi mepesi na kuepuka kukaa juani kwa muda mrefu inapowezekana.
Joto la usiku litakuwa la wastani huku likitarajiwa kufikia takribani nyuzi joto 25°C, mchanganyiko wa mchana wenye joto na usiku wa wastani ni wa kawaida katika msimu huu na unatarajiwa kuendelea kwa wiki nzima.
Upepo wa wastani unatarajiwa katika maeneo mengi. Mwanzoni mwa wiki, upepo unaweza kuwa mkali kidogo, lakini utapungua kadri wiki inavyoendelea. Ingawa upepo huu unaweza kupunguza joto la mchana, unaweza pia kuongeza vumbi katika maeneo makavu na kuathiri miundombinu au vitu vyepesi.
Hali ya bahari inatarajiwa kuwa tulivu hadi wastani, hali inayofaa kwa shughuli za kawaida za baharini kuwa mufti. Hata hivyo, bahari inaweza kuwa na mawimbi ya wastani katikati ya wiki, hasa katika maeneo ya maji makuu.
Kutokana na hali hiyo, tahadhari inahimizwa kwa shughuli za bahari ya uwazi kama vile uvuvi, usafiri wa majini na shughuli za kibiashara katika maji makuu. Wakazi wa maeneo ya pwani wanashauriwa kufuatilia taarifa za kila siku za hali ya hewa, kuhakikisha usalama wao na kuepuka kuingia baharini wakati wa mawimbi makubwa.
Kwa ujumla, hali ya hewa inatarajiwa kuwa yenye ukavu na joto jingi kwa wiki nzima, huku kukitarajiwa mvua nyepesi za asubuhi katika maeneo machache. Chukua tahadhari dhidi ya joto kali hasa wakati wa mchana.
Endelea kufuatilia taarifa zaidi na tunakutakia wiki njema, salama na yenye mafanikio.