Chama cha Orange Democratic Movement, ODM, kimekanusha taarifa zinazosambaa kwamba kinara wa chama hicho Raila Odinga,ako Hali mbaya ki afya.
By Dayo Radio
Published on 06/10/2025 09:16
News

Chama cha Orange Democratic Movement, ODM, kimekanusha taarifa zinazosambaa kwamba kinara wa chama hicho Raila Odinga,ako Hali mbaya ki afya.

Kupitia taarifa iliyotolewa siku ya Jumapili, chama hicho kimesema uvumi huo hauna ukweli wowote, kikibainisha kuwa Raila alisafiri nje ya nchi Ijumaa kwa shughuli rasmi.

ODM imeeleza kuwa kama Raila angekuwa ana matatizo ya kiafya, angejulisha wananchi kama ambavyo amekuwa akifanya hapo awali alipolazwa hospitalini mwaka 2010 akiwa Waziri Mkuu, na mwaka 2021 alipogunduliwa kuwa na virusi vya corona.

Chama hicho sasa kimelaumu upande wa upinzani unaoongozwa na Rigathi Gachagua kwa kusambaza uvumi huo, kikidai ni njama ya kudhoofisha nguvu za kisiasa za serikali ya Rais William Ruto.

Vile vile ODM imekashifu wapinzani wake kutumia mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kueneza taarifa za uongo, zikiwemo picha zilizotengenezwa kwa teknolojia ya AI.

Chama hicho kimetoa wito kwa Wakenya kupuuza uvumi huo, kikisisitiza kuwa Raila Odinga yuko salama na mwenye afya njema.

Comments
Comment sent successfully!