KEJUSTA YAPINGA TABIA YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI ILIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA IKULU.
By Dayo Radio
Published on 13/09/2025 14:18
News

Chama cha walimu wa Shule za sekondari msingi (KEJUSTA) kimepinga vikali tabia iliyojitokeza kwa baadhi ya walimu wa shule za msingi wakati wa kikao kilichonyika Ikulu kilichohudhuriwa na Rais.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari chama hicho kimesema kuwa katika kikao hicho, walimu hao walidaiwa kumzomea Katibu Mkuu wa KUPPET, Bw. Akello Misori, alipokuwa akizungumzia masuala yanayohusu walimu na wanafunzi wa shule za sekondari za junior.

KEJUSTA aidha kimeeleza kwamba tabia hiyo ilikuwa ya aibu, isiyo na heshima kwa taaluma na iliyoashiria dharau kwa mazungumzo ya kimaendeleo.

Hata hivyo chama hicho kimefafanua kuwa kitendo hicho kilikuwa njama ya kukandamiza hoja halali na kuzuia msukumo wa kudai uhuru wa shule za junior. Kimesisitiza kuwa kitasalia thabiti na kuendelea kushinikiza kujitegemea kwa shule hizo katika miundo, uongozi na usimamizi.

Aidha, KEJUSTA kimeonya Chama cha Walimu wa Shule za Msingi (KNUT) na was

Comments
Comment sent successfully!