MWENYEKITI WA MUUNGANO WA PWANI AKEMEA MATAMSHI DHIDI YA VIONGOZI WA DINI YA UISLAMU
By Dayo Radio
Published on 11/08/2025 13:50
News

Mwenyekiti wa muungano wa viongozi wa kidini Pwani Patriotic Religious Leaders, Sheikh Abu Qatada, amemtaka  aliyekuwa naibu wa Rais, Rigathi Gachagua, kuomba msaha kufatia matamshi yake ya kuhusisha dini ya kiislamu na kundi haramu la kigaidi la 

Al-Shabaab.

Haya yanajiri baada ya Gachagua kudai kwamba viongozi wa dini ya kiislamu waliokuatana na rais William Ruto kaunti ya Mandera kwa ajili ya mipango wa kutoa vikwazo vya usajili wa vitambulisho katika maeneo ya mipakani hawakuwa viongozi wa kidini bali walikuwa wanamgambo wa Al-Shabaab akitaja kauli hiyo italeta uchochezi wa vita vya kidini humu humu nchini na kuvuruga amani na usalama wa taifa.

“Kauli hii ni ya uchochezi na haina ushahidi wowote. Maneno kama haya yanaweza kuchochea chuki na mgawanyiko miongoni mwa Wakenya. Namtaka Gachagua aombe msamaha hadharani kwa jamii ya Kiislamu na wananchi kwa jumla. Taifa la Kenya ni takatifu na tunapaswa kudumisha mshikamano wa kitaifa.”

Aidha amewataka viongozi wote wa kisiasa kuepuka kutoa matamshi yanayoweza kudhoofisha mshikamo wa taifa na badala yake kuwataka washirikiane na viongozi wa dini ili kuimarisha amani.

 

Na HARRISON KAZUNGU.

Comments
Comment sent successfully!