Ni afueni kwa vijana kutoka Kaunti ya Mombasa baada ya serikali kutangaza kurejesha kazi mitaani iliyositishwa kwa njia ya sintofahamu. Hatua hii inatarajiwa kupunguza changamoto za ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana na kuwawezesha kushiriki katika shughuli za kijamii na maendeleo ya mtaa.
Akizungumza hapo Jana katika uwanja wa tononoka kaunti ya Mombasa huku akiendesha hafla ya kuwaezesha kina mama,naibu rais profesa kithure kindiki,amesema kwamba programu ya kazi mtaani itaanza ndani ya mwezi huu ili kuhakikisha vijana wanapata ajira na kujikuza kiuchumi.

"Programu ya Kazi Mtaani inaanza ndani ya mwezi huu ili kuhakikisha vijana wanapata ajira na kujikuza kiuchumi."
Naibu Rais aliongeza kuwa serikali imetenga rasilimali maalum kwa ajili ya kuhakikisha utekelezaji wa programu hiyo unakuwa wa haraka na wenye matokeo ya kudumu akiisitiza kwamba mpango huo pia unahusisha mafunzo stadi za kazi na ujasiriamali ili kuwapa vijana uwezo wa kujiajiri baada ya kuhitimu kwenye programu.
Haya yanajiri siku chache baada ya serikali kubadili nia na kuanza kusikiliza matakwa ya vijana, ikiwemo kuwaalika Ikulu na kuahidi kuwawezesha kupitia miradi mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na kimazingira. Hatua hii inapokelewa kwa matumaini makubwa na wadau wa maendeleo katika Pwani.
NA HARRISON KAZUNGU.