Mbunge wa Kaloleni, Kaunti ya Kilifi, Paul Katana, ameitaka serikali kushughulikia changamoto zinazowakumba wakaazi wa Pwani.
Akizungumza katika hafla ya kuchangisha fedha kwa vikundi vya kina mama na vijana iliyofanyika katika uwanja wa Tononoka hapo jana Kaunti ya Mombasa, Katana amesema tangu taifa lipate uhuru, wakaazi wa eneo hilo bado wanaishi maisha duni kutokana na ukosefu wa ajira kwa vijana na miundombinu ya kimaisha huku akisisitiza ufufuzi wa viwanda ndio utakaoleta suhuluhu la kudumu kwa wapwani.
“Tangu taifa lipate uhuru, wakaazi wa eneo hili bado wanaishi maisha duni kutokana na ukosefu wa ajira kwa vijana na miundombinu ya kimaisha. Ufufuzi wa viwanda ndio utakaoleta suluhisho la kudumu kwa wapwani.”

Watikati uohuo mbunge huyo amelaani vikali vitendo vya unyakuzi wa ardhi za pwani na akisema hali hiyo inawanyima wakaazi fursa ya kutumia rasilimali zao na kuwafanya waishi katika hali ya uskota.
“Ninalaani vikali vitendo vya unyakuzi wa ardhi za Pwani kwani hali hiyo inawanyima wakaazi fursa ya kutumia rasilimali zao na kuwafanya waishi katika hali ya uskota.”
NA HARRISON KAZUNGU.