“Tutalinda Bahari zetu kwa Mkono wa Sheria”Asema Thoya.
By Dayo Radio
Published on 06/08/2025 12:15
News

Naibu Gavana wa Kaunti ya Mombasa, Francis Thoya, atoa wito kwa wakazi wa kaunti hiyo kuacha mara moja tabia ya kutupa taka ovyo katika bahari na maeneo ya fukwe, akisisitiza kuwa mazingira safi ya baharini ni msingi wa uchumi na maisha ya jamii ya Pwani.

 

Akiwahutubia wanahabari mapema leo katika kongamano lililowaleta pamoja washikadau mbalimbali katika sekta ya bahari mjini Mombasa Thoya atangaza msimamo mkali dhidi ya wale wanaohujumu juhudi za kulinda mazingira ya bahari.

 

“Mtu yeyote anayechafua bahari kwa kutupa taka au kuharibu mikoko atachukuliwa hatua kali za kisheria. Hatutakubali mazingira yetu kuendelea kuharibiwa,” asema Thoya kwa msisitizo.

 

Aidha, ametaja mikoko inaumuhimu mkubwa katika kuhifadhi mazingira ya pwani na kuitaka jamii kushirikiana na serikali kuendeleza upandaji wa mikoko kama njia ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

 

“Kupanda mikoko si kazi ya hiari bi ni jukumu letu la pamoja. Ni njia ya kujilinda sisi, uchumi wetu, na maisha ya vizazi vijavyo,” aongeza Thoya.

 

Hata hivyo naibu Gavana huy ameeleza kuwa serikali ya kaunti ya Mombasa inaweka sheria madhubuti na inaongeza ufuatiliaji ili kuhakikisha kuwa mazingira ya bahari yanalindwa ipasavyo kwa manufaa ya jamii yote.

 

NA HARRISON KAZUNGU.

Comments
Comment sent successfully!