MAADHIMISHO YA MAANDAMANO.
By Dayo Radio
Published on 25/06/2025 12:22
News

Maandamano ya Juni 25, 2025 ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu vijana wa GenZ kuuawa kikatili na polisi yameaanza kwa amani katika baadhi ya kaunti humu nchini.

 

Katika Kaunti ya Mombasa, waandamanaji hao wamefika kwa wingi na kuoneka wakibeba mabango yaliyoandikwa jumbe za kudai haki huku wakitembea kwa umoja bila vurugu.

 

Baadhi ya picha zilizo pepereshwa na video zilizopeperushwa zaonyesha waandamanaji wakiwa katika shughuli zao bila kuvurugana na maafisa wa polisi waliokuwa wakiimarisha usalama.

Kwa upande mwingine, maandamano hayo pia yameanza kwa amani katikati mwa jiji la Nairobi huku nyimbo za kudai haki kwa waathiriwa wa ukatili wa polisi zikitawala.

Hata hivyo, kadri watu walivyoongezeka katikati mwa jiji la Nairobi ndivyo maafisa wa usalama walivyoongezwa ili kukabiliana na waandamanaji hao.

Katika Kuanti ya Kisumu, maandamano hayo pia yameaanza kwa amani huku waandamanaji wakidai haki kwa wale waliouawa mikononi mwa polisi.

Maandamano hayo pia yameonekana kushika kasi katika kaunti za Embu, Machakos, Uasin Gishu, Makueni, Nakuru, Nyeri, Kajiado na Kisii.

Comments
Comment sent successfully!