TAIFA LA KENYA LAKANUSHA KUHUSIKA KATIKA VITA VYA SUDAN.
By Dayo Radio
Published on 16/06/2025 15:54
News

Serikali ya kenya imekana madai ya kuhusika katika vita vinavyoendelea katika Taifa la Sudan.Akiwahotubia waandishi wa habari mapema Leo jijini Nairobi,msemaji wa serikali Daktari Isaac Mwaura ametaja kuwa Taifa la Kenya liko mbioni kuwanusuru na kuwasaidia wakimbizi waliotharika kutokana na vita hivyo huku akitaja kwamba kupitia Kwa ushirikiano wa muungano mataifa IGAD wameahidi kutoa kima cha dolla miliiioni 2 zitakazo saidia kupiga jeki walioathirika kutokana na vita hivyo.

Vile vile amesema kwamba Taifa la Kenya liko tayari kupokea makundi yyote ya kivita yanayozuru Kenya Kwa kutafuta ushauri na suluhu ya kudumu 

"Tunaahidi kutoa kima cha shilingi milioni 2 ili kuwasaidia waathiriwa wa vita hivyo na taifa la Kenya lipo tayari kupokea wengine wanaohitaji ushauri wa namna ya kutatua matatizo ya nchi"

 

Aidha amesema ipo haja Taifa kuunda sera na Sheria itakayosaidia waandamanaji kutengewa sehemu maalum ya kuandamana ili kuepuka vurugu na uharibifu Mali unaotokana na maandamano.

"Lazima tuwe na sheria itakayosaidia waandamanaji kuwa na sehemu yao maalum itakayosaidia kulinda biashara za wananchi"

Comments
Comment sent successfully!