Afisa mkuu wa kituo cha polisi cha Central Samson Taalam na afisa wa polisi James Mukhwana wanataka mashtaka dhidi ya mauaji ya mwanablogu Albert Ojwang kusitishwa.
Katika ombi la mahakamani wawili hao wametaja kukamatwa kwao kama ukosefu wa sheria wakisema kuwa uchunguzi ungefaywa kwanza kabla ya mchakato wowote wa kisheria dhidi yao kuanzishwa.
Aidha wanasema kuwa vifo vinavyotokea katika seli vinahitaji kufanyiwa uchunguzi wa kina kama ilivyo kwenye sheria ya kifungu cha 385 hadi 388 cha sheria ya jinai.
Kulingana nao kukiukwa kwa sheria hiyo kunaathiri mchakato wa sheria na kuhujumu harakati za kutafuta haki.Vilevile Taalam amedai kuwa walikamatwa na maafisa wa kutathmini utendakazi wa polisi IPOA hali ambayo ni kinyume na taratibu za kisheria.
Haya yanajiri huku IPOA ikiomba kuzuiliwa kwa Taalam kwa siku 21 ili kutoa nafasi ya uchunguzi zaidi kufanyika.