IJM YAKASHIFU MAUAJI YA FARIDA KADZO
By Dayo Radio
Published on 12/06/2025 13:04
News

Shirika la international Justice Mission limeapa kushirikiana na familia ya Farida Kadzo Changawa msichana anayedaiwa kuuwawa kwa kudungwa kisu na kijana mmoja anayedaiwa kuwa mpenzi wake kaunti ya Kilifi hadi pale haki ya msichana huyo itakapopatikana.

 

Akizungumza na waandishi mapema Leo mjini Mombasa meneja wa shirika Hilo Aggrey Juma amesema kwamba atahakikisha familia ya Faridah inapata Haki ili iwe funzo kwa wengine hatua itakayosaidia kukomesha visa vya dhulma za kijinsia vinavyoendelea kushuhudiwa nchini.

" Sisi kama shirika tumesikitishwa na kifo cha mwanadada msichana ambaye bado alikuwa ni mtoto wa miaka kumi na saba ambaye aliuliwa wiki iliyopita siku ya ijumaa,kama shirika tutafatilia kesi kuhakikisha kwamba haki imetendeka kwa hii familia na kwa niaba ya Farida ili wengine ambao wanajipata katika hali kama ile alikuwa wanasaidika."

 

Kulingana na Rose Kitheka shangaziye marehemu,Farida mwenye umri wa miaka 17 aliuwa kwa kudungwa kisu kooni mnamo tarehe 6 mwezi juni mwaka huu na kueleza kuwa msichana huyo ameacha mtoto mdogo wa miezi tisa.

Kufikia sasa familia hiyo inalilia haki ya mpendwa wao huku ikitaka serikali kumchukulia hatua za kisheria mhusika mkuu wa mauaji hayo.

Comments
Comment sent successfully!