Kampuni za vijana,wanawake na watu wenye ulemavu kupewa kandarasi Kwale.
By Dayo Radio
Published on 05/06/2025 13:25
News

Gavana wa Kaunti ya Kwale, Fatuma Achani, ameagiza idara zote kumi za kaunti kutoa kandarasi za miradi ya maendeleo kwa kampuni zinazomilikiwa na wanawake na vijana pekee. 

 

Kwa mujibu wa gavana huyo, miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa zahanati, vituo vya elimu ya awali yani (ECDE), upanuzi wa mabomba ya maji na usafi wa miji katika maeneo ya Diani, Kinango na Lunga Lunga, hatua ambayo imelenga kupunguza ukosefu wa ajira na umaskini kwa wakaazi wa Kwale. 

 

Hata hivyo,kampuni zaidi ya 300 za vijana na wanawake zimesajiliwa, huku 105 kati ya hizo zikipewa kandarasi za kuchimba visima na kusambaza vifaa vya serikali.

 

 Aidha Gavana Achani pia ametoa wito kwa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum kushirikiana kimakundi na kujisajili ili kupata nafasi za kushiriki katika zabuni za kiserikali na za kibinafsi.

 

By Millicent Mtanah

Comments
Comment sent successfully!