Washikadau wa dini ya kiislamu kaunti ya Mombasa wamejitokeza na kuja na kunzisha mchakato wa kitaifa wa kuwafunza waislamu masomo ya dini.Akizungumza katika kongamano liliowaleta pamoja washikadau wote wakiwemo mafisaa na watalaamu wa uundaji wa mtaala.
Afisaa kutoka Jamlick Gitonga amesema kwambq mtaala huo utasaidia pakubwa jamii ya waislamu kupata vyeti ambavyo vitatambulika na serikali

na kutoa wito kwa vijana kuchagua taasisi ambazo zina kubalika na serikali ili kuepuka udanganyifu wa utoaji vyeti ghushi.
"Kama serikali tupo tayari kuwaongoza ili jamii ya waislamu wamepata mtaala unaotambulika na setikali na kuhakikisha wanapata masomo yanayofaa"
Kwaupande wake mwenyekiti wa muungano wa pwani patriotic religious Sheikh Abu Qatada amepongeza hatua hiyo na kutaja kuwa elimu pekee ndiyo itakayosaidia kuendesha taifa na hata kuwakomboa vijana kutokana na maovu.
"Ni hatua kubwa kwa jamii ya waislamu na tukiwa na ushirikiano na serikali kama tutapata kutambulika kama wengine wanavyo amvulika"