Mwenyekiti wa muungano wa pwani patriotic religious leaders (PPRL) ,sheikh Abu Qatada amekosoa vikali matamshi ya aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua aliyetamka hivi majuzi.
Akizungumza katika kikao na wanahabari mapema Leo Mombasa kiongozi huyo amelaani matamshi hayo na kumtaka Gachagua kuomba wakenya msamaha la sivyo serikali iingilie kati na kumchukulia hatua Kali za kisheria.

"Tuna laani maneno ya Bwana Rigathi Gachagua na ajitokeza tena mara ya pili, aombe wakenya msamaha la sivyo ,tunaomba serikali ichukue hatua na serikali imchunguze mtu kama huyu, ana ajenda fiche nyuma ya maneno kama haya kwasababu ni maneno machafu na tumesikitishwa sana na tunaona mtu kama huyu ni hatari kwa hii nchi mtu ambaye kwamba anataka kuturegesha miaka ambayo kwamba tulishuhudia vurugu"
Aidha kauli hiyo imeungwa mkono na mwanaharakati wa kutetea Haki za kibinadamu Mombasa,Faridah Rashid na kuwataka vijana kutotumika vibaya na baadhi wanasiasa wanaotaka kusambaratisha amani uwiano wa Taifa.
"Mimi nawaomba watoto wangu mkae na muangalie haya mambo yanavyokwenda na sisi mama zenu ndio tunaumia zaidi msisikilize maneno ya wanasiasa potofu hata kidogo"
Haya yanajiri siku chache zilizopita baada ya gachagua kusema kwamba huenda kukashuhudiwa machafuko ya uchaguzi wa mwaka wa 2027 iwapo matokeo ya uchaguzi huo hayatakuwa ya huru na Haki.