MADZAYO AKOHOA KUHUSU ODM.
By Dayo Radio
Published on 02/05/2025 12:30
News

Seneta wa Kilifi Stewart Madzayo,ameshikilia kuwa chama cha ODM hakijaingia serikalini akitetea hatua ya baadhi ya viongozi wa chama hicho kuteuliwa kwenye baraza la mawaziri.

Kulingana na Madzayo,ODM iliingia mkataba na serikali ya Kenya Kwanza kwa lengo la kushirikiana ili kuhakikisha kenya inakuwa na amani na inapiga hatua kimaendeleo.

Kiongozi huyo wa wachache katika bunge la seneti pia amesifia utendakajikazi wa mawaziri walioteuliwa kutoka chama cha ODM.

Wakati huo huo Seneta huyo amesema kuwa viongozi wa ODM wataendelea kuikosoa serikali kwa mujibu wa katiba.

Aidha Madzayo amebainisha kuwa chama hicho kitakuwa na mgombea wa urais kwenye uchaguzi mkuu wa 2027.

"Hatuwezi kuacha chama cha ODM ambacho kiko na sifa chungu nzima na mizizi ya kutosha na tunawahakikishia wakenya lazima tutakuwa na mgombea wa urais ifikapo mwaka wa 2027"

Comments
Comment sent successfully!