Wizara ya afya chini ya bodi ya kuthibiti madawa na sumu imetoa ilani kwa wakenya kutotumia dawa aina ya paracetamol huku wakitilia shaka kiwango cha ubora wake.Akitoa ilani hiyo hapo Jana mkurugenzi wa bodi hiyo Daktari Fred Siyoi, amesema kwamba dawa hizo zinazotoka katika kampuni ya dawa ya Kamla Amurut kutoka India zinaonyesha dalili ya kubadilika rangi na kutilia shaka ubora wake Kwa ajili ya usalama wa wakenya.

Hata hivyo Siyoi ameweza kuorodhesha aina tatu Kwa makundi 3 zinazopatikana Kwa miligramu1000 na mililita100 kupitia njia ya sindano zikiwemo lumidol injection nambari cm4594007,cm4594008,cm4594009.
Blink injection nambari,
cs459405,cs4594004 na
Paragen injection nambari K4290027.