NPS YAMUONDOLEA HOFU GACHAGUA.
By Dayo Radio
Published on 16/04/2025 12:48 • Updated 16/04/2025 12:49
News

Idara ya polisi imemtaka aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kutoa taarifa kwa polisi kuhusu ratiba na mienendo yake ili kuruhusu maafisa kupanga ulinzi wake ipasavyo.

Kupitia taarifa rasmi, Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja alimhakikishia Bw Gachagua kuwa, wakenya wote wanastahili ulinzi. Awali Gachagua alikuwa amedai kuwa kuna njama ya kumuua.

“Kwa kuzingatia hofu ya usalama aliyotoa Bw Gachagua, anashauriwa kushirikiana na polisi wa viwango vyote iwapo atahitaji ulinzi zaidi na kutoa taarifa mapema kuhusu ratiba na shughuli zake za hadhara ili kuwezesha mipango na uratibu wa kiusalama,” ilisema taarifa ya NPS.

Ikumbukwe kwamba Jumanne asubuhi Gachagua alitoa madai mazito dhidi ya serikali, akisema kuna mpango mahususi uliosukwa wa kutaka kumuua.

Katika barua yake, Gachagua alimlenga moja kwa moja Inspekta Jenerali, akimshutumu kwa kuondoa walinzi wake, hali iliyomweka kwenye hatari tangu alipoondolewa madarakani.

Hata hivyo, NPS ilisisitiza kuwa hali ya usalama nchini iko shwari na kuwa kuna mikakati ya kuzuia uhalifu

 

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online