UTATA WA CHAMA CHA UDA MOMBASA.
By Dayo Radio
Published on 15/04/2025 14:18
News

Viongozi wa chama cha UDA tawi la Mombasa wamemsuta vikali mbunge wa nyali Mohammed Ali Kwa matamshi yake  aliyotamka Jana ya kuendelea kumuunga mkono aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua.

Wakizungumza katika makao makuu ya chama hicho tawi la Mombasa ,viongozi hao wamemtaka mbunge huyo iwapo ako na azma ya kujiondoa kutoka Kwa chama hicho atumie njia mwafaka pasi na vurugu.

Wakiongozwa na  mkurugenzi wa chama hicho Mutungwa Wambua amemkosoa kiongozi huyo Kwa kushindwa kupeleka malalamishi katika kamati husika na kujiweka njia panda iwapo yuko kwa chama au amejiondoa.

""Tulikuwa tumeeka mikakati ya kueka vile mambo yanatakikana yawe ila yeye yuaenda kwa media anaongea vitu tofauti tuhitajitumuelewe kama yupo ama yuatoka"

Wakati uo huo mratibu wa programu na kampeini za UDA Fatma Baryan amemtaja Mohamed Ali kama kiongozi  mtalii wa kisiasa asiyekuwa na msimamo thabiti.

"Huyu jamaa hana msimamo kama kiongozi hafai kuwa na hali hiyo"

Vile vile mwenye kiti wa chama hicho Khamisi kitaka, amemtaka mbunge huyo iwapo Ako na azima ya kujiondoa katika chama kufanya hivyo mara Moja bila kuzua utata na kuharbia jina chama cha UDA. 

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online