Mkuu wa Utumishi wa Umma na wafanyikazi wa Ikulu Felix Kosgei amewahiza wahusika walioboboea na maswala ya kiteknolojia kukoma kutumia mitandao kwa njia isoyofaa akijata inahatarisha maisha ya wakenya.Akizungumza katika uzinduzi wa kongamano liliowaleta pamoja wanachama cha ukaguzi na udhibiti wa mifumo ya habari ISACA mjini Mombasa Koskei amesema ni wakati sasa taifa kukumbatia njia za kidijitali ili kurahisisha utekazi.
"Tunaona sasa mambo mengi yamebadilika na niwakati taifa kuliinua kutumia Teknolojia wale wote waanaohusika na taaluma katika Teknolojia lazima wahusishe wengine ili watu wawe na uwazi zaidi"
Aidha ametaja tayari serikali imetenga kiwango cha fedha kitakachosaidia kuboresha na kuwarahisishia wakenya wanaotafuta huduma za kiserikali kwa njia inayofaa na hata kukomesha ufisadi.
"Ningependa kusema kwamba mambo mengi sasa yatakuwa sawa hasa pale wakenya watakuwa wanatafuta huduma sa kiserikali kwani tumetenga kima cha pesa ambacho kitatumika kuziba mianya yote ya ufisadi."
NA HARRISON KAZUNGU.