Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amewataka wakaazi wanaoshi karibu na jengo hatari linaloporoka eneo la Kona ya kilifi Bondeni Mombasa kutoka eneo hilo ili kupeana nafasi ya ubomozi.Akizungumza na waandishi wa habari gavana Nassir,amesema shuhuli za ubomozi wa jengo hilo litaanza kesho na kutekelezwa na kikosi cha jeshi KDF.
"Hili jumba litabomolewa na jeshi na amri iliyoko ni kwamba mtu yeyeyote asikae ndani ya nymba yake ambaye yupo karibu na jengo hilo na hata sehemu za kuabudu"
Hata hivyo kiongozi huyo amesema wanaendelea kumtafuta mtu Mmoja anayekisiwa huenda alikwama katika jengo hilo.
"Inakisiwa kwamba huenda kukawa kuna mwili wa mtu mmoja uliokwama kulingana na kamera za CCTV pia ningeomba wagonjwa wote ambao wako hali mahututi katika hospitali ya Makadara wahamishwe katika sehemu salama."
Wakati uo huo gavana amethibitisha kuwa hospitali kuu ya makadara itaathirika pakubwa kutokana na ubomozi na kutoa amri ya wagonjwa walio hali mahututi kuhamishwa katika sehemu iliyo