USALAMA WAIMARISHWA PWANI.
By Dayo Radio
Published on 07/04/2025 14:06
News

Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomeni ameanza ziara yake ya siku sita kutathimini hali ya usalama ukanda wa pwani.

 

Akizungumza na waandishi wa habari hapa mjini Mombasa waziri murkomen amewahakikishia wakaazi wa pwani na watalii wanaozuru Mombasa usalama wa kutosha .

Waziri huyo aidha amesema asasi za usalama zimeweka mikakati ya kutosha kukabiliana na magenge na makundi ya uhalifu ambayo yamekuwa yakitatiza usalama pwani.

"Kila mmoja anajua vile ukanda wa pwani unapitia changamoto za mangenge ya kiuhalifu na Kenya kwa ujumla kutoka MRC mpaka PANG BOYS ambao wamekuwa wakihangaisha wakaazi na tunamiango dhabiti ambayo tumeeka na mengine tayari inatekelezwa kwa hivyo tunawakikishia wakaazi mambo yatakuwa sawa"

Wakati uo huo Murkomen amekanusha madai ya kuvamiwa kwa watalii na kundi la vijana la panga boys,huku akisema ni mtalii Mmoja aliyepokonywa simu na kijana mmoja wa kuranda randa mitaani.

"Kwa ujumla ni kwamba swala la usalama wa watalii lazima tuliengalie kwa makini sana na sasa tunawahikishia watalii wanaozuru humu nchini wanapata usalama"

Kadhalika waziri Murkomen amedhibitisha kuachiliwa huru kwa machifu waliotekwa nyara na wanamgambo wa alshabaab kaunti ya Mandera.

Ziara ya waziri huyo ukanda wa pwani inajiri huku visa vya utovu wa usalama vikiripotiwa kuongezeka jambo ambalo limezua hofu na taharuki kwa wakaazi na pia wageni wanaozuru pwani wakati huu wa likizo ya pasaka.

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online