Kizaazaa kimeshuhudiwa katika mkutano wa Mamlaka ya Mazingira NEMA hapa Mjini Mombasa baada ya mkurugenzi mkuu wa kituo cha Haki,Utawala na masuala ya mazingira (CJGEA) Phyllis Omido na maafisa wengine kuzua tafrani na Kusababisha kutibuka kwa mkutano huo.Akizungumza na waandishi wa habari Omido amedai kuwa licha ya kwamba walishinda kesi dhidi ya mamlaka ya NEMA katika mahakama ya upeo kuhusu uchafuzi wa mazingira mtaa wa Owino Uhuru, bado kuna jaribio na njama ya kutotii amri ya Mahakama hiyo ambayo katika uamuzi wake iliitaka Mamlaka ya NEMA kulipa CJGEA milioni 700.
"Tulishanda kesi dhidi yao na wanapaswa kulipa kima cha takribani shilingi milioni 700 kwahivyo Neema waache kudangaya wanainchi."
Mkurugenzi huyo amesema kuwa kama kituo cha Haki, Utawala na masuala ya mazingira kitawachukulia hatua kali za kisheria maafisa wote wa NEMA wanaokaidi amri ya mahakama na kutaka kuendesha zoezi la kushirikisha umma kinyume cha sheria badala ya kulipa milioni 700 walizoamrishwa na mahakama.
"Wanapasa kuchukuliwa hatua hatutakubali tena neema waendelee kuhadaa umma na wakenya kwa ujumla na tutawakatama ili na kuwachukulia hatua za kisheria"
Kwa upande wake Khamis Mbiyo mmoja wa waathiriwa wa kemikali hiyo hatari ya LEAD eneo hilo la Owino Uhuru amesema kuwa athari za kemikali hiyo zingali zinashuhudiwa katika jamii ya eneo hilo huku zikisababisha maafa na ulemavu kwa wakaazi wa eneo hilo.
"Wananchi wanaumia na kulia wanapoza maisha yao nyinyi neema kawzi ni kukaa maofisini tu na kula pesa ya mkenya anayetozwa ushuru hili jambo lazima likome"
Huku Mamlaka ya NEMA ikitarajiwa kuendesha mchakato wa kupokea maoni ya wananchi eneo hilo la Owino Uhuru, maafisa wa CJGEA wakiongozwa na Phyllis Omido wameapa kukabiliana na NEMA kisheria hadi pale Haki itakapotendeka kwa waathirwa.
Haya yanajiri huku Mamlaka hiyo ikipania kufanya kikao na wananchi wa Owino Uhuru Alhamisi hii kufuatia maamuzi ya mahakama kuhusu usafishaji wa maeneo hayo yaliyoathirika na kemikali ya lead iliyosababisha majeruhi mbalimbali kwa wakazi wanaoishi maeneo hayo.