Viongozi wa dini ya kiislamu na wale wa kijamii wametoa wito Kwa jopo la kuteua makamishna wa wakfu kuteua majina ya wakilishi kutoka eneo la pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema Leo mjini Mombasa, mwenyekiti wa shirika la PWANI PATRICK LEADERS sheikh Abu Qatada, amesema kwamba majina yaliorodheshwa na jopo la kuteua makamishna 5 ,hakuna hata mwakilishi Mmoja kutoka eneo la pwani licha ya asilimia 99 za wakfu nchini zinatoka ukanda wa pwani.

"Katika majina ya watu 5 hakuna jina la mtu anayetoka katika eneo la pwani tunaomba wapwani pia waweze kuwakilishwa vyema."
Hata hivyo kiongozi huyo amepinga dhana ya kwamba pwani Kuna changamoto ya elimu inayochangia wa pwani kusalia nyuma katika uteuzi wa nyadhfa mbalimbali.
"Tunao viongozi wasomi wa eneo la Pwani na haiwezekani pwani nzima tukose mtu wa kutuwakilisha kilio chetu ni tupate wawakilishi kama wengine walivyowakilishwa"
Wakati huo huo Qatada ametoa wito Kwa wazazi na asasi za usalama kuwajibika katika kupambana na utovu wa usalama unaoshudiwa Kila uchao eneo la pwani.