Mashirika ya kutetea haki za kibanadamu mjini Mombasa Haki Afrika na Muhuri, wamekashifu ongezeko la magenge ya wahuni almaharufu 'panga boys' hususani mwezi huu mtukufu wa ramadhan.
Akizungumza na waandishi wa habari , Afisa wa wa kitengo cha dharura Haki Afrika Mathias Shipeta, amesema kwamba ni sharti maafisa wa polisi kuwajibika na kuwakabidhi vijana hao huku wakifwata Sheria za kikatiba .

"Ni lazima polisi wachukue hatua ya kuwadhibiti vijana wanaohangaisha wakaazi wa kwale na Mombasa kwa maana hilo ni jukumu lao la kuhakikisha mwananchi anapata usalama bora"
Hata hivyo kauli hiyo imeungwa mkono na Afisa wa shirika la Muhuri Francis Ouma huku akiwanyoshea kidole cha lawama baadhi ya maafisa wa polisi kwa kukosa maadili na kushirikiana na magenge hayo.
"Tushuku sana kunaushirikiano kati ya mangenge ya kiuhalifu na polisi wadogo kwani tunafahamu wakubwa wao hawanashida ila hawa wa chini ndio tatizo ndio maana hata wahuni hawana wasiwasi"
Hata hivyo Ouma ametoa onyo Kwa maafisa wanaotumia nguvu kupita kiasi kukabiliana na wahalifu kwamba watakabiliwa na mkono wa Sheria.