Ni afueni kwa waumini wa dini ya kiislamu wasiojiweza kupata msaada wa chakula kwa hisani ya halmashauri ya bandari ya Mombasa KPA.Akizingumza katika hafla ya kuzindua zoezi la mgao huo wa chakula kwa mashirika 19 yanayotetea haki za waumini wa diniya kiislamu wasiokuwa na uwezo,mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya bandari ya Mombasa Willam Ruto, amesema zoezo hilo limegharimu kima cha takriban shilingi million 4.56 kwa ajili ya kuhakikisha familia zisizo na uwezo wanasherehekea na wenzao bila changamoto yoyote.
"Tunafurahi kutoa msaada huo utakaosaidia jamii ya kislamu na pia kuleta ushirikiano utasaidia jamii kwa ujumla"
Hata hivyo ametaja zoezi hilo kama la kuweka nyuso za tabasam kwa wasiojiweza hususani Msimu huu wa sherehe unapokarbia.
"Tumeona ni vyema kuonyesha moyo wa upendo kwa ndugu zetu waislamu kwa maana hali ya utoaji si rahisi lakini kama jamii ni lazima tugawanye chochote tulicho nacho"