WANAUME WATATU WAKAMATWA KWA KUMPIGA MWANAMKE ALIYEDINDA KUWEKA MICHANGA KABURI LA MUMEWE
By Dayo Radio
Published on 25/03/2025 12:29
News

Maafisa wa polisi wamewatia mbaroni wanaume watatu waliohisika katika kumdhulumu mwanamke mmoja baada ya kukataa kumwaga mchanga kwenye kaburi la mumewe huko Nyabisimba kaunti ya Nyamira.

Washukiwa hao Robert Pokea Sarudi,Bismark Ondiek Sarudi na Lameck Ogindo Osoro wamekamatwa huko Mwongorisi baada ya uchunguzi wa kisa hicho kilichotokea tarehe 21 mwaka huu kukamilika.

Kulingana na maafisa wa usalama mwanamke huyo alidhulumiwa alipohudhuria mazishi ya mumewe baada ya kualikwa na familia ya marehemu na baadaye kulazimishwa kumwaga mchanga kwa kile kinachodaiwa kuwa tamaduni za wakaazi wa eneo hilo.

 

picha kwa hisani

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online