Wito umetolewa kwa viongozi kote nchini kuwa na ushiriakiano dhabiti katika utendakazi wao.
Akizungumza hapa Mombasa mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya ambaye pia ni naib mwenyekiti wa walio wengi katika bunge la Kitafa amesema kuwa umoja wa viongozi ndio utaoleta maendeleo kwa kwa wakenya na wala sio kulengana.

"Tunaona chama cha UDA ni chama ambacho kinajumuisha kila mmoja na itakuwa vyema sisi kama viongozi kuhakikisha tunafanya kazi kulingana na vile inafaa ili kuleta maendeleo kwa wakenya"
Aidha ameshukuru rais William Ruto kwa kukhakikisha kuwa wapwani wengi wanapata nafasi na nyadhafa mbalimbali serikalini akitaja itasaidia pakubwa katika kuleta amani nchini.
"Ningetaka pia vile vile kumpongeza mtukufu rais kwa kutupatia watu wetu nafasi za zikiwemo zile za ukatibu kwani haijawahi kutokea katika taifa letu tukufu la kenya"