SITAJIUZULU BILA SABABU
By Dayo Radio
Published on 23/03/2025 07:51
News

Waziri wa utumishi wa umma Justin Muturi aapa kutojiuzulu licha ya shinikizo kutoka Kwa baadhi ya viongozi serikalini.

Akizungumza hapo Jana mjini Mombasa baada ya kufungua kongamano la muungano wa mataifa barani Afrika,muturi amesema kwamba alimwandikia barua rais William ruto na kutoa sababu zake za kutohudhuria Baraza la mawaziri Hadi atakapopata jibu kuhusu swala la utekaji nyara.

"Nilimuandikia rais sababu zolinifanya ambazo zilinifanya nisihudhirie na swala zima ni lile la utekaji nyara vijana na sasa ningali nasubiria jibu maana swala la watu kuteswa limekuwa janga kubwa humu nchini"

Hata hivyo amedokeza kwamba haoni sababu zozote zitakazomshawishi kujiuzulu na kamwe hatajiuzulu Kwa kusema ukweli.

"Mtu lazima azungumze ukweli na niko tayari kama kuna makosa ya kusema ukweli kujitetetea."

Haya yanajiri baada ya viongozi serikalini akiwemo kiongozi wa wengi bungeni Kimani Ichungwa na kiongozi wa wachache bungeni Junet Mohammed kumtaka waziri muturi kujiuzulu mara Moja.

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online