MLO WA RAMADHANI
By Dayo Radio
Published on 17/03/2025 14:36
News

Ni afueni sasa kwa familia zisizojiweza hapa mjini Mombasa baada ya serikali ya kaunti kupokea chakula cha msaada kutoka kwa shirika la AMSONS GROUP linaloshirikiana na kampuni ya saruji ya Bamburi Cemment.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kupokeza chakula hicho mwakili wa shirika hilo Rajab Sumba amesema chakula hicho kitaganywa kwa watoto kutoka familia kwa zisizo na uwezo ili kuwasaidia wakati huu wa mfungo wa ramadhani.

"Sisi tuko tayari kushirikiana na viongozi wa kaunti ya Mombasa na pia jamii ili tuzidi kuinua maisha ya wengine na pia tutakaa chinj na tuangalie ni wapi jamii inahitaji zaidi"

Kwa upande wake waziri wa utalii na utamaduni wa kaunti ya Mombasa Mohamed Osman ameeleza kuridhishwa kwake na hatua iliyochukuliwa na shirika hilo na kusema na kusema kwamba wataendelea kushirikiana na shirika hilo  na kuhakikisha familia zisizojieweza zinaishi katika hali ya usawa kama familia zengine hususan msimu huu wa ramadhani.

"Sisi kama viongozi wa Mombasa kaunti tutahakikisha familia zote zisizo jiweza katika mji huu wa Mombasa zinatambuliwa na kuwa kama familia zengine."

 

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online