Afisa wa baraza la kudhibiti maambukizi ya virusi vya ukimwi Douglas Bosire amesema kuwa dawa za kuzuia kupata virusi vya ukimwi PREP zitatolewa kwa wanawake wajawazito pekee.
Afisa huyo amesema kuwa hatua hiyo itasaidia wanawake wajawazito kuzuia virusi kuwafikia watoto tumboni.
Haya yanajiri baada ya rais wa Marekani Donald Trump kusitisha ufadhili wa baadhi ya miradi nchini ikiwemo sekta ya afya mnamo mwezi January mwaka huu.