MWANGAZA AONA GIZA
News
Published on 14/03/2025 by Dayo Radio

Ni pigo kuu kwa gavana wa Meru Kawira Mwangaza baada ya mahakama kuu kuidhinisha uamuzi wa bunge la Seneti wa kumuondoa gavana huyo mamlakani.

Uamuzi huo umejiri baada ya bunge la Seneti kupiga kura kwa kauli moja na kuidhinisha malalamishi yaliowasilishwa na bunge la kaunti ya Meru dhidi ya kiongozi huyo.

"Kulingana na Kifungu cha 181 cha Katiba, Kifungu cha 33 cha Sheria ya Serikali ya Kaunti na Kanuni ya Kudumu ya 86 ya Kanuni za Kudumu za Seneti, Seneti imeazimia kumwondoa afisini kwa kumwondoa madarakani mheshimiwa Kawira Mwangaza, Gavana wa Kaunti ya Meru na gavana huyo kukoma kuhudumu," Spika Amason Kingi amesema.

Baadhi ya mashtaka yanayomkabili Kawira ni kwamba alikiuka kanuni za katiba, utumizi mbaya wa ofisi ya umma, ubadhirifu wa fedha za umma miongoni mwa mashtaka mengine.

Ikumbukwe kuwa hii ilikuwa mara ya tatu kwa Mwangaza kung'olewa madarakani kufikia Seneti tangu achaguliwe afisini Agosti 2022.

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online