Waziri wa Leba Alfred Mutua ametangaza mpango mpya wa kuajiri wafanyakazi kupitia mpango wa Kazi Majuu.
Kulingana naye zoezi hilo la kuajiri litafanyika katika kanisa la Jesus Winner Ministry liliko huko Roysambu, Nairobi, kati ya Machi 5 na Machi 6 2025.
Mutua aidha amesema hayo ni kwa mujibu wa ahadi ya Rais William Ruto ya kuimarisha fursa za nje ya nchi.
''Kufuatia ahadi ya rais Dkt William Ruto ili kuimarisha usafiri wa wafanyikazi na na kuwapa fursa za ng'ambo KAZI MAJUU kwa vijana wetu, kutakuwa na zoezi la kuajiri vijana hao katika kanisa la Jesus Winner Ministry, Roysambu, Kaunti ya Nairobi mnamo Jumatano, Machi 5 na Machi 6 2025, kuanzia saa 8 asubuhi hadi 5 PM,'' alisema kwenye mtandao wake wa kijamii.

Miongoni mwa nafasi za kazi zilizo na nafasi ni wauguzi ambao wana digrii akitaja waataajiriwa kazi nchini Ujerumani, Saudi Arabia, Qatar, Dubai na Australia.
Wengine ni madereva ambao wana leseni ya kuendesha gari (Wamiliki wa Leseni wa Ex GCC wanahimizwa sana kujisajili) na waendeshaji mizigo katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).