Mwili wa afisa aliyefariki nchini Haiti kutarajiwa kuwasili nchini wiki hii.
Published on 03/03/2025 16:09
News

Matayarisho ya kusafirisha mwili wa Afisa wa polisi aliyepigwa risasi Haiti yamekamilika na mwili wake watarajiwa kufika nchini Kenya kati ya tarehe 4 na 6 mwezi huu Kwa maandalizi ya mazishi huko kaunti ya kajiado.

 

Akizungumza katika ibada kanisani kajiado mashariki,inspekta jenerali wa polisi Douglas kanja amemuombeleza Afisa huyo kama shujaa aliyekuwa mstari wa mbele kupigania Haki za wananchi wa Haiti.

Vile vile mkuu wa polisi huyo ametoa risala zake Kwa familia ya mwendazake akiwemo mjane aliyeachwa na watoto wawili .

"Tumepoteza afisa mwema aliyekuwa Haiti akiendeleza juhudi zake za kuhakikisha kuwa kuna amani na usalama eneo hilo.Alifarika akiwa kwenye mstari wa mbele na tunajivunia kwa kuwa alikuwa kijana mdogo aliyekuwa tayari kutumikia taifa na popote pale.Familia tunasema pole sana,kwa majirani tunasema pole sana,majirani poleni na hata mjane awe pole sana."

Haya yanajiri baada ya serikali ya kenya kutuma vikosi vya usalama kukabiliana na magenge ya wahalifu nchini haiti kama njia ya kudumisha usalama na kuhakikisha amani imerejea.

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online