Ikiwa leo ni siku ya kuadhimisha siku ya walemavu wanaotumia viti vya magurudumu kote ulimwenguni hapa Mombasa hafla hiyo imeweza kufanyika katika ofisi za muungano wa watu wanaoishi na changamoto za kimaumbile nchini (APDK) iliyoko eneobunge la Changamwe.Kulingana msimamizi mkuu wa muungano wa watu wanaoishi na changamoto za kimaumbile Eva Njoroge wametumia siku hii ya leo kusambaza na kunganya viti vya magurudumu kwa wenye changamoto za kutembea akitaja vitawasaidia pakubwa katika shuhuli zao za kila siku.
"Leo tumekuja hapa Mombasa kuhakikisha tunagawanya viti hivi vya magurudumu kwa watu wanaoishi na changamoto za kimaumbile kwa wale wasioweza kutembea ili kuwatia moyo."
Hata hivyo Bi.Eva ameiomba jamii kutowaficha watoto wenye changamoto za kimaumbile ili wakaweze kutambulika na kupata usaidizi unaofaa.
"Ninawaomba sana wazazi na hata jamii kwaujumla isiwafiche watu wenye changamoto za kimaumbile kwa sababu sivyema na kufanya hivyo ni kuwanyima kati ya haki zao ikiwemo hata upande wa elimu."
Aidha ameitaka serikali kuja na mbinu mwafaka na kuhakikisha mijengo yote inayojengwa humu nchini ijengwe katika hali itakayofamfa mtu mwenye changamoto ya kimaumbule kutumia bila matatizo.
"Viongozi wote na serikali kwa ujumla ni lazima wahakikishe kuwa mijengo yote inayojengwa inajengwa katika hali inafaa ili kumfanya mtu mwenye changamoto ya ulemavu kupta huduma katika mijengo hiyo.
NA HARRISON KAZUNGU.