ONYO LA UCHOMAJI WA MISITU NCHINI.
Published on 28/02/2025 13:51
News

Huduma ya Misitu humu nchini (KFS) imesitisha uchomaji wa mimemea isiyofaa karibu na misitu.

Kulingnagana na mkuu wa hifadhi za misitu Alex Lemarkoko amesema watu wote wanaonuia kuchoma mimea karibu na hifadhi za misitu lazima watoe taarifa ya maandishi saa 48 kabla kwa hifadhi za misitu au kwa kituo cha Polisi kilicho karibu. 

"Huduma imeimarisha utayari kwa kupeleka vifaa vya ziada vya kuzima moto, magari 12 ya pick-up, na carrier sita za askari, pamoja na kuwaita wafanyakazi wote walio kwenye likizo ili kuimarisha na kujieka katika utayari wa mikasa ya moto," amesema Lemarkoko katika taarifa yake kwa vyombo vya habari. 

Aidha amefichua kuwa KFS imeweka mfumo wa kutambua dalili  kufuatilia mioto ya misitu katika maeneo ya Mlima Kenya, Aberdares na Mau.

Hata hivyo amebainisha  kuwa tangu Januari 2025, moto mkubwa ulioripotiwa ni kutoka Isiolo, Garissa, na mifumo ya na baadhi ya sehemu za pwani.

"Kwa hakika, kumekuwa na ongezeko kubwa la matukio ya moto wa misitu ndani ya wiki iliyopita," Lemarkoko Amesema. 

Kituo cha Amri cha KFS kimerekodi matukio 180 ya moto ambayo yamesababisha zaidi ya hekari 1,357.97 za mimea ndani ya misitu iliyotangazwa na gazeti la serikali katika maeneo kadhaa ya hifadhi kuharibiwa.

Shirika hilo la misitu limesema kulingana na tathmini ya hatari ya moto iliyofanywa katika kaunti mbalimbali, ni wazi kuwa nchi iko katika msimu wa moto wa misitu unaotarajiwa kuendelea hadi katikati ya Machi.

Mhifadhi huyo amethibitisha kuwa KFS inashirikiana kikamilifu na Mashirika ya kijamii ya Misitu, umma, Huduma ya wanyamapori ya Kenya, mashirika ya serikali ya kitaifa na kaunti, na washirika wengine wa uhifadhi katika juhudi zinazoendelea za kuzima moto.

Mnamo Januari, KFS ilitangaza hatua za kujitayarisha kwa mikasa ya moto ili kupunguza, kuhakikisha natukio yagunduliwa  mapema na majibu ya haraka yatolewe iwapo moto utazuka, ikiwa ni pamoja na utunzaji na uondoaji wa vyanzo vyote vya moto katika msimu wote.

 

NA HARRISON KAZUNGU

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online